Watanzania Waaswa Kujiunga na Bima za Afya

No comments

Asilimia 27 ya watanzania pekee kati ya watu million 53 waliopo nchini ndiyo wanatumia bima ya afya jambo ambalo ni hatari kwa jamii huku ukizingatia maradhi ni sehemu ya mwanadamu.

Serikali nchini imeendelea kutoa kipaumbele katika huduma za afya zenye ubora na zinazowafikia wananchi wote ili kuboresha afya zao ikiwa ni njia pekee ya kutambua umuhimu wa afya bora kwa wananchi wake kwani afya bora ni raslimali muhimu kwa maendeleo.

katika kuhakikisha kuwa wananchi wana afya bora, serikali imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutoa huduma za afya kwa kuzingatia sera na miongozo iliyopo ambapo jana taasisi ya bima ya afya ya Jubelee kwa kushirikina na wadau wengine wamezindua bima mpya itakayo mwezesha mtanzania wa chini kuweza kupata huduma za kiafya.

Edward Mbanga ni kaimu mkurugezni wa sera na mipango toka wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto ameishauri jamii kujiunga na bima za afya ili kuepukana na matatizo pindi wakihitaji huduma kubwa wakati wakiwa wagonjwa.

No Comments Yet.

Leave a comment