Wachezaji watano Wanaowania tuzo ya mchezaji bora VPL 2016/17

No comments

Wachezaji watano wameteuliwa  kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu wa  Mwaka 2016/2017.

Walioteuliwa kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho ni

  • Aishi Manula kutoka (Azam FC),
  • Haruna Niyonzima wa (Yanga African),
  • Mohamed Hussein (Simba Sc),
  • Shiza Kichuya (Simba Sc)
  •   Simon Msuva (Yanga African).

Majina hayo yatapigiwa kura na makocha, makocha wasaidizi na manahodha wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara pamoja na wahariri wa michezo kutoka vyombo mbalimbali vya habari za Michezo nchini.

Wahusika watatumiwa fomu maalum za kupiga kura kwenye E-mail za klabu zao na vyombo husika vya habari. Mwisho wa kupiga kura ni saa 6 usiku ya Jumanne, Mei 23 mwaka huu.

Hafla ya kutoa tuzo hiyo ambayo inaratibiwa na Kamati ya Ushauri ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itafanyika Mei 24 mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

No Comments Yet.

Leave a comment