Valencia Wasitisha Usajili Wa Nemanja Maksimovic

No comments

Meneja wa klabu ya Valencia  Cesare Prandelli, amezima mipango ya usajili wa kiungo kutoka nchini Serbia na klabu ya Astana Nemanja Maksimovic.

Prandelli, amefuta mpango huo kwa kuamini fedha zilizokua zimetengwa kwa ajili ya kiungo huyo zitatosha kumsajili mshambuliaji wa mabingwa wa soka nchini Italia Simone Zaza, anaecheza kwa mkopo West Ham Utd.

Prandelli, amesema amefanya maamuzi hayo baada ya kutafakari kwa kina na kuona hakuna haja kubwa ya kufanya usajili wa mchezaji anaeitumikia nafasi ya kiungo wakati wa majira ya baridi (Januari 2017), kutokana na uwepo wa wachezaji kadhaa kikosini mwake ambao wanaweza kucheza sehemu hiyo.

Amesema ameona ni bora akajipanga kwa ajili ya kuboresha safu yake ya ushambuliaji ili kukamilisha mpango wa kutimiza malengo aliyojiwekea kwa msimu huu wa 2016/17.

Image result for Simone Zaza
Simone Zaza.

“Zaza ni mchezjai muhimu,” Alisema Prandelli.

“Maksimovic ni mchezaji mzuri pia tena ana umri mdogo, lakini nimeona kuna haja ya kumuacha ili kutoa nafasi kwangu kuboresha nafasi ya ushambuliaji ambayo ina umuhimu mkubwa kuelekea mwezi Mei 2017.

Maksimovic alitarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa mwanzoni mwa juma lijalo, na tayari mazungumzo ya kuondoka kwa mkopo yalikua yamefikia pazuri.

No Comments Yet.

Leave a comment