Unamjua vizuri Waziri Mkuu mteule wa awamu ya 5 Kassim Majaliwa? hii hapa historia yake

19 comments

Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John P Magufuli, leo ametegua Kitendawili cha nani atakuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya 5 kwa kumteua Mh Kassim Majaliwa.

Kassim Majaliwa ni Mbunge aliyetokea katika Chama cha Mapinduzi CCM, akiwakilisha jimbo la Ruangwa Lililopo mkoani Lindi.

Mpaka leo anateuliwa, Mh Majaliwa anateuliwa kuwa Waziri mkuu alikuwa Naibu Waziri TAMISEMI.

‘Professional’ yake hasa ni mwalimu, aliwahi pia kuwa katibu wa Chama cha Walimu mkoa, mkuu wa Wilaya, na nyadhifa nyingine tele za kuwahudumia wananchi.

Kwa kiasi kikubwa baadhi ya Wabunge wakongwe wa Chama cha Mapinduzi, wameonesha kuwa na imani na Mh Kassim Majaliwa.

Amezaliwa December 22 mwaka 1960 na mpaka hivi sasa ana umri wa miaka 54, na ana Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

19 comments

 1. Gadenia Msigwa

  Hata Sijawahi kumwona hata siku moja

  • Lazaro,manoti

   Naamini katika waziri mkuu wa awamu wa 5,hata hivyo tasnia ya ualimu hutoa vitu vyema

 2. phelick msemwa

  akafanye kaz apigane na ufisadi

 3. razack omary

  perfect, anafaa#hapa kazi tu.

 4. Danny kasuka

  Wana ccm wote tunaweza hata angeteuliwa diwan wang ibrahim angefanya tuu!

 5. Akaze buti

 6. izizigga

  Kama Hamfahamu historia ya mtu msiwe mnakurupuka. Mhe. Majaliwa hajawahi kuwa mkuu wa wilaya ya Singida

 7. KASSIM sisi watanzania tunakutegemea kwani sifa zako zinasitaili kufanya kazi tunakuombea MUNGU akuepushie balaa Amina

 8. heri mlaponi

  binafc nimefurah sana kuckia hvyo na wilaya yang kutoa wazr mkuu

 9. filbert honde

  Sawa tumemuona kilichobaki ni kazi tu

 10. DR. SANGWA

  Mungu amuongoze kufanya kazi kwa uadilifu.

 11. mikidadi

  Mungu amlinde juu ya majukum take na awe muadilifu…

 12. Abdalasa

  Mmmmmmhhh…
  ndio kwaaaaanza na msikia kwa vyombo vya hamali.
  Haya kwel #mabadiliko ya kweli.

 13. Damas Mapunda

  Looking at his background profile, the man can deliver! Let’s just give him the required support.

 14. Denis Akulu

  Huyu si Majaliwa, ni Magufuli mwingine!

 15. James marco

  Nina imani na uteuzi wa Rais hivo wazir mkuu afanye kazi kwa manufaa ya Taifa na si kwa manufaa ya watu wachache tu.

 16. Huyu Ni Jembe Letu Aisee.

 17. Francis msangi

  Kweli huyu jamaa anafaa kabisa kuwa wazir mkuu na tunategemea mabadiliko kutoka kwake

Leave a comment