SUMATRA Yapewa Mwezi Mmoja Kuondoa Taka Ngumu Zilizopo Kando ya Barabara

No comments

Naibu waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais,muungano na mazingira Luhaga Mpina ametoa mwezi mmoja kwa mamlaka ya usafirishaji majini na nchi kavu(SUMATRA) kuhakikisha wanaondosha taka ngumu zote zilizozagaa kando ya barabara.

Akizungumza ofisini kwake mjini dodoma mara baada ya kupokea taarifa za utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa mwezi Disemba mwaka jana kutoka baraza la mazingira la taifa(NEMC) na SUMATRA Mpina amesema pamoja na taasisi hizo kutekeleza maagizo yake ipasavyo kuna mambo lazima wayatekeleze.

Aidha amemtaka mkurugenzi wa NEMC na mkurugenzi wa mazingira kuandaa muongozo wa utupaji taka na wahakikishe wanausambaza ndani ya miezi miwili ili kuondoa sintofahamu ya nani anapaswa kusimamia na kujua taka zinapopelekwa mara baada ya kutolewa bandarini au melini.

Kwa upande wao meneja leseni barabara Leo Ngowi,Meneja usajili,ukaguzi na udhibiti kutoka SUMATRA mhandisi Alfred Waryana na afisa mazingira mkuu kutoka NEMC Blandina Cheche wamesema wamepokea malekezo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi katika kuhakikisha wanazingatia usafi wa mazingira

Hatua hiyo imekuja mara baada ya kubaini uwepo wa taka ngumu katika barabara zinazotupwa na wenye mabasi na vyombo vingine vya usafiri na hivyo kusisitiza kusimamia sheria iliyopo kwa kuwapiga faini watakaokiuka.

No Comments Yet.

Leave a comment