Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Lawakaribisha Wawekezaji Nchini

No comments

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limewakaribisha wawekezaji mbalimbali wa viwanda kuja kuwekeza nchini kwani kwasasa wameweza kuboresha Zaidi miundombinu yao ambapo upatikanaji wa gesi unaweza kupatikana kwa urahisi Zaidi.

Akizungumana waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa TPDC Mhandisi Kapulya Musomba amesema kuwa kutokana na ujenezi mpya wa bomba la gesi lililojengwa kwasasa upo uwezekano mkubwa wa viwanda vingi kujengwa.

Aidha Mhandisi Musomba amesewasihi watu binafsi ambao niwafanyabiashara kuhimiza watu wanje kuja kuwekeza nchini ili kufikia dhima ya serikali ya viwanda.

Mhandisi Musomba amesema kuwa kwasasa wamejipanga katika mkoa wa Dar es Salaam kibiashara Zaidi ili watanzania waweze kunufaika na gesi hiyo kwa kuweza kumiliki biashara kubwa na zenye tija kwa Jamii.

No Comments Yet.

Leave a comment