Nigeria waongoza Listi ya Wanamuziki Matajiri Afrika.

3 comments

Pengine ulikua unajiuliza ni Mwanamuziki gani tajiri kuliko wengine Barani Afrika. Kampuni ya utafiti ya Answers Africa inakuletea horodha ya Wanamuziki kumi wanaongoza kwa utajiri Afrika, huku Nigeria ikiongoza na kufuatiwa na Kongo DRC.

Namba moja ni Youssou N’Dour , Ni moja kati ya Wasanii wakubwa Afrika, ambapo mziki wake umeegemea zaidi
kwenye asili ya Afrika na anatoka nchini Senegal.

Namba mbili inakamatwa na P Square, Wanamuziki hawa mapacha kutoka nchini Nigeria wanakamata nafasi ya pili. Peter na Paul wamekua wanafanya vizuri kwenye kazi yao ya muziki tangu walipotoka kwa mara ya kwanza kwenye Tasnia hii.

Kwenye listi hiyo namba tatu imekwenda kwa D’banj Msanii mwngine kutoka nchni Nigeria, D’banj alijizoelea umaarufu kwa kibao chake cha Fall in Love, huku namba nne ikienda kwa mkongwe wa muziki wa dansi na rhumba Koffie Olomide wa DRC Kongo.

Salif Keita ni jina lenye heshima kubwa nchni Mali na barani Afrika kwa ujumla. Mwanamuziki huyu anafanya muziki wa asili na anaingia kwenye listi hii akishika nafasi ya tano.

Kutoka DRC Kongo, mkali mwingine wa muziki wa dansi Fally Ipupa anaingia anakamata nafasi ya sita na kumuacha 2 Face Idibia kutopka Nigeria akikamata nafasi ya saba.

Nafasi ya nane imekwenda kwa Hugh Masekela kutoka nchini Afrika Kusini, na nafasi ya tisa imeshikwa na Bank W mwanamuziki kutoka Nigeria huku Jose Chameleon akiwakilisha ukanda wa Afrika Mashariki kwa kumata nafasi ya kumi.

3 comments

  1. Uledi almaa

    Tanzania hata mmojaaaaaa!!!!!! kumbe mzikii bado xi biaxhara…..# bongo

  2. lameck daudi

    Ataivyo nasisi vijana wetu wanazidi kutuinua! Kikubwa tusikate tamaa kusapoti nyumbani.

  3. list ya wasanii wa bongo hatuione coz tunaham ya kutaka kujua wasanii wetu matajiri bongo

Leave a comment