Nasari,Mwakyembe Washikana mashati bungeni

No comments

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe Kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Joshua Nasari na Bungeni Tarehe 19 mwaka huu  wawashiana moto  na kusababisha mzozo mkubwa katika mjadala uliokuwa ukiendelea.

Wabunge  hao walihamisha Maada ya hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kuanza kujadili  suala la Richmond ambalo lililotokea mwaka 2008, huku Mbunge Nasari akimtuhumu Waziri  Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa.

“Huyu Mwakyembe ndiye aliyeongoza ripoti ya Richmond na hakumpa nafasi mheshimiwa Lowasa ajitetee, leo tena kapewa dhamana ya kuongoza Wizara ya Habari, Nape Nnauye ameondolewa lakini hakuna nafasi ya kumhoji Mkuu wa Mkoa… hakuna haki hapo,” alisema.

Kauli za Nasari zilimfanya Waziri  Mwakyembe kuomba mwongozo na aliposimama alisema: “Nilikuwa naongoza kamati na utaratibu mzuri wa kisheria ni kuwa, kama utaona kuna ushahidi wa kutosha hakuna sababu ya kumuita mtu, unaleta taarifa bungeni halafu Bunge linakuja kuamua.”

Dk Mwakyembe alisema katika taarifa yao, waliona hakuna sababu ya kumuita Lowassa kuhojiwa kwani ushahidi ulikuwa wazi na ndiyo maana hakutakiwa kuitwa mbele ya kamati badala yake walikuja kumshtaki bungeni.

“Huyu mtu wanayekuwa na mahaba naye kwa sasa, nasema wamlete hata leo waone kama hatutamnyoa kwa chupa, kanuni za kibunge zinaruhusu anaweza kuirudisha tena taarifa ya Richmond na ikaanza upya,” alisema Waziri  Mwakyembe.

No Comments Yet.

Leave a comment