Mwili wa Marehemu Dkt. Elly Marko Macha Waagwa Bungeni leo

No comments

Mwili wa aliyekuwa mbunge wa viti maalum (CHADEMA) marehemu Dkt. Elly Marko Macha umeagwa leo katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Dkt. Elly Marko Macha ambaye alizaliwa mwaka 1962 na kufariki mwa huu 2017

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanauaga kuuaga  mwili huo na baadae kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Mkoani Arusha. Marehemu Dkt. Elly Macha alikuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Dkt Macha alimefariki katika hospitali ya New Cross, Wolverhampton nchini Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu, Macha aliyekuwa mlemavu wa macho tangu akiwa mtoto wa miezi mitano, amefariki akiwa na umri wa miaka 55 .

Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi Amen.

No Comments Yet.

Leave a comment