AM SORRY JK YAMPELEKA NIKKI MBISHI BASATA

No comments

Rappa Nikki mbishi ameitwa na Baraza la sanaa nchini (BASATA) kuhojiwa juu ya wimbo wake wa Am sorry Jk aliutoa mwishoni mwa mwezi wa January

Nikki ameweka wazi hayo kupitia ukurasa wake wa instagram na kudai kuwa aliitwa BASATA tarehe 09 February lakini alishindwa kwenda kwakua alikukwenye msiba wa mama yake mkubwa nje ya Dar es salaam

Hiki ndicho alichoandika Nikki kupitia Instagram yake
Salaam Tanzania,Afrika na Dunia!
Leo tarehe 13/02/2017 nimehitajika kuripoti ofisi za BASATA ambapo wanadai walinitumia ujumbe zaidi ya siku 3 nyuma ila sikuwa hewani labda kwa sababu ya msiba ulionipata, kufuatia ujumbe niliyotumiwa juzi tarehe 09/02/2017 kwa njia ya msg za kawaida za simu ya kiganjani ambapo
ujumbe umesema hivi “Habari za jioni?Tafadhali fika bila kukosa BASATA kesho 10/02/2017 saa tatu kuzungumzia mustakabali wa wimbo wako wa ” I AM SORRY JK”
Nimeomba niripoti leo kufuatia kuchelewa kufika kwa ujumbe huo.
Unadhani nini kitatokea?Mi sifahamu ninachofahamu ni Itika wito kataa neno.
Asanteni na Mungu awabariki nyote.
#TagWaTanzania
#TagWaTanzania #TAGVIUMBEHAIWOTE #TAGVIUMBEHAIWOTE

No Comments Yet.

Leave a comment