Akon Awaburuza Wasanii wa Afrika , Listi ya wasanii wenye Mkwanja Mrefu afrika

No comments

Jalida la Forbes Afrika limetoa majina kumi ya wasanii wa afrika wenye pesa zaidi huku msanii Akon akiwa ameshika namba moja akiwabwaga wasanii wengine tisa

AKON

Akon ameuza Albamu zake million 35 katika ulimwengu , Ameshinda tuzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na tuzo tano za kuteuliwa za Grammy na amekuwa mara 45 Billboard katika nyimbo bora 100. Ameshika nafasi ya kwanza kwa wasanii wenye Mkwanja mrefu Afrika kutokana na Utafiti wa jarida la Forbes Afrika.

BLACK COFFEE, SOUTH AFRICA

Nkosinathi Maphumulo ndo jina lake kamili na nimsanii aliyewahi shinda tuzo mbalimbali , Amezaliwa katika nchi ya Afrika ya kusini katika familia inayojihusisha na muziki ya KwaZulu-Natal (KZN) , ndiye anayeshika namba mbili katika wasanii kumi wa Afrika wenye Pesa Nyingi.

HUGH MASEKELA, SOUTH AFRICA

Hugh alizaliwa Witbank, Mashariki mwa Johannesburg , Ameachia albumu 43 na kutumbuiza na wasanii kama Marvin Gaye, Dizzy Gillespie, The Byrds, Fela Kuti, Paul Simon, Stevie Wonder na Miriam Makeba anashika nafasi ya Nne

DON JAZZY, NIGERIA

Don Jazzy ni moja wa matajili Afrika na ni wakwanza kwa Nigeria, jina lake kamili ni Michael Collins Ajereh na alianza kufanya mziki toka akiwa mdogo kanisani .

TINASHE, ZIMBABWE-AMERICAN

Tinashe ni binti mwenye umri wa miaka 24 ambaye amewahi kuwa katika filamu ya Cora Unashamed na hata sauti yake kutumika katika kutengenezea cartoon vile vile aliweza kushiriki katika Filamu ya The Polar Express na kushinda tuzo ya Oscar katika Uigizaji yeye ameshika nafasi ya tano.

JIDENNA, NIGERIAN-AMERICAN

Jidenna Theodore Mobisson Msanii anaye kuja na moto wa kuotea mbali ambaye aliambiwa na baba yake kuwa awe Injinia kupitia Forbes Afrika imempa nafasi ya sita kati ya wanamziki wenye pesa ndefu Afrika

WIZKID, NIGERIA

Wizkid ni msanii ambaye ametamba na anazidi kutamba kimataifa ambapo alichomoza na kibao cha Ojuelegba ambapo kili wika sana ndani na Nje ya Afrika , Kanasa namba saba katika wasanii wenye mkwanja Mrefu Afrika

DAVIDO, NIGERIA

Davido ni moja ya wasnii maarufu na amewahi sema kati ya watu waliomfanya aamini kuwa anaweza kuwa staa na ikawezekani ni P-Square na D’Banj ,alidai 2012 album ya “Omo Baba Olowo” ilimtoa.

SARKODIE, GHANA

Michael Owusu Addo alianza kwa kuwa msanii anaye imba muziki wa kufoka foka na akiwa ni msanii chipukizi akipewa msaada na Meneja Duncan Williams, ni msanii wa Ghana ambaye amezaliwa katika kijiji cha Kpanlogo,  ‘Mewu, Ni wimbo wake wa kwanza kati ya Albamu 14 ambao aliuza takribani nakala  4,000 siku ya kwanza  alivyoiachia na Nimsanii wa kwanza Ghana kushinda tuzo za BET award Anashika nafasi ya tisa kuwa Msanii wa Afrika tajili

OLIVER MTUKUDZI, ZIMBABWE

Oliver Tuku Mtukudzi ana albums 65, ambazo ni nyingi kumshinda Marehemu Michael Jackson na Whitney Houston. Ambazo amefanya miaka 41 anashika nafasi ya 10 kwa wasanii wa Afrika wenye pesa

No Comments Yet.

Leave a comment