M2 The P:Ninaudai Muziki Pesa Nyingi sana

No comments

Mgaza Pembe M2 The P Msanii anayetamba na Kibao cha ‘Ukiwa Mzuri Nakuhonga ‘  Asema Anaudai muziki wa Bongo Pesa nyingi sana kutokana na kazi alizo fanya kwani bado haujamrudishia Pesa za Kutosha japo kuwa Ameugharamia  kwa pesa nyingi sana .

 M2 The P Akihojiwa na 100.5 Times Fm aeleza sababu ya kuchora Chata (Tatoo) kwenye Mwili wake  kwa kusema

 “Nilichora Tatoo ya kwanza Mara baada ya Kumpoteza Mama Yangu mzazi ambapo nilichora Chozi  na Tatoo ya Pili Nilichora Chozi tena Likiwa linawakiliza kifo cha Albert Mangwea

Msanii M2 The P alisema Anazidi kumkumbuka Albert Mangwea kwani  alikuwa ni zaidi ya rafiki Msanii huyo alisema

Kaobama Ni Pacha yangu na ndomaana nimechora Taswira ya Sura yake katika Kifua changu na kuandika maneno ya faraja ambayo hunifariji kila siku

Aidha aliweza kuwazungumzia baadhi ya Watayarishaji wa muziki Hususani Mr.T-touch ambaye ndiye anaye mtengenezea muziki wake kila siku Kwa kumpa shukrani zake za dhati kwani nyeye ndiye Producer ambaye anamfanyia muziki wake Bure kabisa bila hata kumchaji Pesa yoyote na kumuhakikishia kuwa Muziki wake lazima ufike mbali

Pia M2 The P Amesema Yeye anajitahidi kufanya muziki kwanza hapa nyumbani  ili akitoka nje iwe Rahisi licha ya kuwa na Conection na watu wengi na kuishi nje ya Tanzania kwa miaka Mingi

 “ Mtu lazima uanze kufahamika kwanza nyumbani ili iwe nyepesi hata unapoenda kumsikilizisha mtu mziki wako  anakuelewa

Wanamuziki wa nje wanajua Kujibrand vizuri na wanatumia nafasi zao vizuri ndiomana tunawaona wamefika hapo walipo , tukiiga mfano wa wenzetu tutafika mbali na muziki wetu wa bongo.

M2 The P Adai ana project nyingi ambazo ziko njiani zinakuja hivyo wapenzi wa muziki wake wakae mkao mzuri kwani kwasasa anafanya muziki usio na Stres hata kidogo , alitaja baaadhi ya wasanii ambao amefanyanao kazi ambazo zitatoka hivi karibuni ni pamoja na TID Mnyama ,Mr Blue, Na Dully na wengine

No Comments Yet.

Leave a comment