WAZIRI NAPE AIPONGEZA TIMES FM KWA KUUNGA MKONO JITIHADSA ZA SERIKALI

No comments

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye leo ameendelea na ziara yake ya kikazi kwenye vituo vya utangazaji kwa kuitembelea Times Radio Fm na kuvitaka vyombo vya habari na vyombo vya serikali kuwa marafiki katika ujenzi wa Taifa bora.

Akizungumza na uongozi na wafanyakazi wa Kampuni ya Times Radio Fm wakati alipotembelea na kujionea utendaji kazi wa kituo hiki na kuipongeza kwa kuandaa vipindi vinavyobeba ajenda ya serikali ya Tanzania ya viwanda .

“ lakini pia nichukue nafasi hii kuwashukuru sana ,jana tulizungumza habari za viwanda na kumbe mlishaanza muda mrefu na niwaahidi kwamba serikali tutakuwa karibu kuhakikisha tunatengeneza mazingira mazuri muda wote “Nape amesema.

Amevitaka vyombo vya habari pindi wanapokutana na mambo magumu kushirikiana kwa ukaribu zaidi na Wizara ya Habari Utamaduni sanaa na michezo sababu wizara hiyo ndio mzazi wa Tasnia ya habari hapa nchini .

Katika hatua nyingine Nape amempongeza Mkurugenzi mkuu wa Times Radio Fm Rehure Nyaulawa kwa jitihada zake za kuunga mkono sheria ya huduma ya vyombo vya habari ya mwaka 2016, kwa kuwasaidia wafanyakazi wake kuongeza elimu, ambapo serikali imeahidi kuanzisha mfuko wa kusaidia wanahabari kwenda kusoma.

Naye Mkurugenzi wa Times Fm ,Rehure Nyaulawa ameeleza dhamira yake ya kubadili baadhi ya vipindi ikiwemo kipindi cha MAISHA MSETO na HATUA TATU venye mrengo wa kutoa elimu kuhusu jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda .

Amesema vipindi hivyo vimeweza kubadili sehemu kubwa ya maisha ya watanzania katika sekta ya ujasiriamali na ujenzi wa viwanda vidogovigogo na kuendelea kutoa elimu zaidi kwa jamii juu ya kazi zinazofanywa na serikali kupitia watendaji wake.

Katika ziara hiyo Mhe. Nape Moses Nnauye ameahidi kuendeleza ushirikiano baina ya Serikali na vyombo vya habari katika utoaji wa habari ambazo ni muhimu kwa wananchi kujua zikiwemo hatua ambalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kutekeleza majukumu yake katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Related Posts

No Comments Yet.

Leave a comment