Sol Campbell Aitabiria Mema Chelsea FC

No comments

Gwiji wa klabu ya Arsenal Sol Campbell amesema klabu ya Chelsea huenda ikatwaa ubingwa wa ligi ya nchini England msimu huu, kutokana na utofauti anaouona.

Campbell amesema kikosi cha Chelsea kimekua na mtazamo tofauti na ilivyokua msimu uliopita, ambapo ilishuhudia wakimaliza katika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi ya nchini England jambo ambalo liliwasikitisha mashabiki wao.

Amesema kutokana na ushindani wa wachezaji kuwania namba katika kikosi cha kwanza pamoja na mbinu za meneja wao mpya Antonio Conte, ndio sababu ambayo imempa nafasi ya kuamini Chelsea huenda watafikia lengo la kutwaa ubingwa.

“Wanakwenda kiuweledi kwa sasa. Wamekamilika katika kila idara,”

“Angalia Leicester – ni vipi alivyofanikiwa kutwaa ubingwa msimu uliopita, walikua kama ilivyo Chelsea ya sasa, kwangu mimi naamini The Blues wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa. Alisema Sol Campbell alipozungumza na mwandishi wa habari wa Sky Sports.

No Comments Yet.

Leave a comment