Rooney Kukosa Mechi Nane.

No comments

Nahodha wa Mashetani Wekundu timu ya Manchester United ya Uingereza Wayne Rooney atakuwa nje ya uwanja kwa wiki sita kutokana na maumivu ya goti aliyopata katika mchezo wa ligi kuu nchini humo dhidi ya Sunderland mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo united ililala kwa mabao 2-1.

Kutokana na maumivu hayo,Rooney pamoja na michezo mingine anatarajiwa kukosa michezo minane ya timu yake katika mashindano tofauti ikiwemo mechi iliyotarajiwa kuchezwa jana usiku katika ligi ya Europa dhidi ya FC Midtjyland iliyopigwa katika uwanja wa Arena Ujerumani.

No Comments Yet.

Leave a comment