PICHA:Shughuli ya Campus Vybez ndani ya Protea Hotel na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri mkuu Vijana, kazi na Ajira Antony Mavunde.

No comments

Elimu ni Mhimili wa Taifa,Kauli mbiu ya Shughuli nzima ya Campus Vybez.

Jumamosi iliyopita Naibu Waziri Anthony Mavule aliweza kukutana na wanafunzi wa vyuo vikuu nakuzungumzia kuhusu changamoto za Ajira kwa vijana Nchini,alipata fursa ya kuongea na wanafunzi hao na pia kujibu baadhi ya maswali ya wanafunzi wao.

Kongamano hilo lililo anandaliwa na kipindi cha Campus Vybez cha TimesFm na watangazaji Raheem na Sandra.Kongamano hili liliwapa fursa wanafunzi kwa ujumla wa vyuo vikuu kongelea matatiza na changamoto wanazopitia kwenye kuomba ajira.

Wageni Rasmi walio alikwa kwenye kongamano hili ni wafanyabiashara na wajasiliamali kama Gibson George, Mjasiliamali Maznat Maza Sinare, Mchekeshaji Mc PiliPili, Reuben Ndimbo Mhadhiri na Mshereheshaji, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri mkuu Vijana, kazi na Ajira Antony Mavunde na Baadhi ya wageni wengine.

Kipindi cha Campus Vybez hurushwa Kila Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa 3:30 usiku.

IMG_3617

Mwanafunzi aliyeuliza changamoto wanazozipitia kwenye kuomba ajira ama field nakuwa ngumu kupata nafasi hizo.IMG_3589 copy

Mmoja wa wanafunzi aliyekuwa akiuliza maswali kwa Naibu waziri Anthony Mavunde.IMG_3457“Usikasirike kuzaliwa katika familia ya kimasikini sio kosa lako, jukumu lako ni kujiondoa katika Umasikini, Mungu kila mtu kampa kipaji angalia jambo gani linajitokeza sana katika maisha yako, usifate mkumbo, niliamua kukifata kipaji changu katika kuchekesha” MC Pilipili ‪#‎ElimuNiMuhimiliWaTaifa‬‪#‎KutokaProteaMudaHuu‬.

IMG_3374copy“Vijana tunaishi katika matumizi makubwa yasiyo na lazima, hakuna kitu kinamtoa mtu kama kusave, nilianza biashara ya Urembo katika Chumba kimoja, nilikuwa navaa nguo mpaka kola inachanika” Mjasiliamali Maznat ‪#‎ElimuNiMuhimiliWaTaifa‬ ‪#‎KutokaProteaMudaHuu‬IMG_3348IMG_3223

Watangazaji wa kipindi cha Campus Vybez Raheem na Sandra wakivunjwa mbavu na MCpilipiliIMG_3299 copy“Nilianzisha 4U Movement nikiwa nimekaa ndani na nikawaambia wenzangu hii itasambaa nchi nzima, Leo inanipa ujasiri wa kuweza kufanya chochote kikafanikiwa kama kijana, 4U tunaviongozi mpaka ngazi ya shina, nawaaminisha vijana wenzangu huu ni wakati wako wa kuyasogelea na kukaribia mafanikio bila kuogopa” Hemed Ali Mwakilishi wa wahitimu Elimu Ya Juu na muanzilishi wa 4U Movement.IMG_3185IMG_3214Wageni kwenye meza kuu Kutoka kushoto ni McPiliPili, Mkurugenzi wa Vipindi Radio TimesFm Bw Ron Fidanza, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri mkuu Vijana, kazi na Ajira Antony Mavunde na Reuben Ndimbo Mhadhiri na Mshereheshaji.IMG_3206 copyIMG_3240“Usikasirike kuzaliwa katika familia ya kimasikini sio kosa lako, jukumu lako ni kujiondoa katika Umasikini, Mungu kila mtu kampa kipaji angalia jambo gani linajitokeza sana katika maisha yako, usifate mkumbo, niliamua kukifata kipaji changu katika kuchekesha” MC Pilipili ‪#‎ElimuNiMuhimiliWaTaifa‬‪#‎KutokaProteaMudaHuu‬.

IMG_3595

Mmoja wa wanafunzi aliyekuwa akiuliza swali kwa Naibu Waziri.IMG_3576

“Muda ni kitu cha msingi na kukitunza sana, nilikuwa na Ndoto ya kuja kuitumikia jamii, nilikataa kazi nyingi za kuajiriwa ili kuifuata Ndoto Yangu, nilikuwa naamini maisha yangu yapo kwenye Siasa, mpaka sasa niliitambua njia yangu na ndio njia niliyopitia” Mgeni Rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri mkuu Vijana, kazi na Ajira Antony Mavunde.

IMG_3689

Mhariri Mkuu wa TimesFm Bi. Melisa Zourha13590493_1118261428253116_5004483108903630235_nTuliandaliwa kuwa mameneja, hatujaandaliwa kujitegemea. Vijana wengi tumejifunga na aina ya elimu ambayo haituruhusu kujitegemea – Gibson GeorgeIMG_3547“Times Fm imejikita kutoa mchango wake kupitia kipindi cha Campus Vibe ili kujenga jukwaa la mazungumzo kwa vijana na wanafunzi wa Elimu ya juu, Pia Times Fm imeanzisha program maalum ili kuwawezesha Wasomi wa Habari Vyuo Vikuu kufanya mazoezi kwa Vitendo” Meneja wa Vipindi Times Fm Ron Fidanza.IMG_3185Baadhi ya wanafunzi walio udhuria Kongamano hilo Protea Hotel.

No Comments Yet.

Leave a comment